Hatimaye Rayon yapata uongozi wa muda

Hayawi yamekuwa, taarifa iliyogonga vichwa vya habari wiki hii kote nchini Rwanda ni kuhusu Munyakazi Sadate aliyekuwa mwenyekiti wa Rayon sports, kamati yake ya uongozi pamoja na wengine wote waliokuwa kwenye mchakato wa migogoro, wote wamesimamamishwa na Dr Kayitesi Usta Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya utawala nchini Rwanda RGB.

Dr Kayitesi Usta Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya utawala nchini Rwanda RGB.

Kuanzia Mei mwaka huu, migogoro ilianza kusikika katika club ya Rayon sports ambapo viongozi wa club hii pamoja na mashabiki baadhi hawakuunga mkono mwenyekiti Munyakazi Sadate, naye kwa upande wake aliwashtaki viongozi wa zamani kwenye ngazi mbali mbali kwa rais wa Rwanda kuwa walitumia vibaya mali ya tim hiyo.

Murenzi Abdallah

Katika mkutano na waandishi wa habari, Dr Kayitesi Usta Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya utawala nchini Rwanda, amesema kwamba kwenye akaunti ya Rayon sports kuna laki mbili faranga za Rwada ikiwa na deni la milioni 800 FRS.

RGB ilifikisha ripoti hiyo katika makao ya Shirikisho la soka duniani FIFA kuhusiana na suala hilo.

Munyakazi Sadate,

Baada ya kusimamishwa kwa viongozi hao wa Rayon Sports, kumefanyika uchaguzi wa kamati ya muda itakayoandaa mabadiliko ya uongozi.
Bodi ya utawala nchini Rwanda (RGB), tayari imeweka uongozi wa muda wa Rayon sport ambayo itaongozwa na Murenzi Abdallah, ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa timu hiyo alipokuwa mkuu wa wilaya ya Nyanza mwaka 2013.

Kamati hiyo ya muda iliyopewa mwezi mmoja ni ya watu watatu Murenzi Abdallah, Twagirayezu Thadee na mwanasheria Nyirihirwe Hilaire.

Miongoni mwa majukumu kamati iliyopewa ni pamoja na kuboresha sheria za jumuiya, kuweka ngazi za jumuiya kwa mujibu wa sheria,kufuatilia shughuli za timu ya Rayon Sports FC siku baada ya siku baada ya siku pamoja na kufuatilia utumiaji wa mali za jumuiya. Timu ya Rayon katika historia yake imeisha twaa zaidi ya vikombe 20.

Aidha Dr Kaitesi amesema kwamba masuala Rayon Sports kama hayatapatiwa ufumbuzi baina yao kwa muda wa mwezi mmoja ujao, RGB ina haki ya kutoa maamuzi ikiwa ni pamoja kusimamaishwa kwa muda.
Christopher Karenzi

Amahoronews.com

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *