Timu mbili za kandanda Rwanda zalalamikia uamuzi wa kushushwa daraja

Baada ya kutoridhika na masharti ya kamati kuu ya FERWAFA kushusha timu za Gicumbi na Heroes katika daraja la pili ya ligi ya Rwanda, timu hizo zimepeleka mashtaka yake kwenye Bodi ya utawala ya Rwanda RGB.

Timu hizi mbili zinadai kuwa ligi ilisitishwa kabla ya mechi 6 kufanyika kutokana na virusi vya corona, Klabu ya jeshi la Rwanda APR FC ilikuwa ikiongoza ikatawazwa mabingwa wa msimu 2019-2020.

Timu za Gicumbi na Heroes ambazo zimerudishwa katika daraja la pili, hazikuridhishwa na uamuzi wa shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA.

Viongozi wa timu hizo wameandikia barua Bodi ya utawala ya Rwanda RGB ili zipewe haki ya kutoshushwa katika daraja la pili zikidai kwamba uamuzi wa kuzishusha haukuwa wa kisheria.

Aidha timu hizi mbili Gicumbi pamoja na Heroes zina sauti moja zikilenga kuwa zimeonewa kurudishwa  katika daraja la pili kama  zilivodhihirisha kwa vipindi tofauti, wanaomba RGB iwatetee.

Hayo yakiarifiwa hatimaye timu ya wananchi Rayon Sports ambayo imekumbwa na matatizo chungu nzima ya uongozi, sasa imefanikiwa kupata viongozi wapya.

Uwayezu Jean Fidele ndiye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa timu hiyo Jumamosi wiki iliyopita,  Kayisire Jacques aliyekuwa kiongozi wa Dream Football Academy, amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Rayon Sports.

Mmpya wa Rayon Sports Uwayezu Jean Fidele baada ya kuchaguliwa amejigamba namna hii.

Rayon Sports mnajua historia yake itaendelea kuwa Gikundiro  forever yaani kipenzi daima, ni timu yetu ni timu ya wanyaranda, ni timu ya nchi kwani inapowakilisha nchi ni ya wanyarwanda.

Mashabiki wametoa mtazamo wao
Jambo la kwanza tumefurahi sana Jean Fidele Uwayezu tunampokea  kama wapenzi wa Rayon sports lakini tunataka abadili mambo  tunahitaji mengi mazuri kuliko wale waliomtangulia.

Huu sasa ni mwanzo wa Rayon Sports wa kutwaa vikombe na kurejesha umoja  wa warayon
Viongozi hawa ni wapya hakuna hata mmoja aliyewahi kuiongoza Rayon miaka iliyopita.

Wadadisi wa mambo wanaona kwamba hali ijayo ya Rayon inaweza kuwa mbaya kwani Wakongwe na waanzilishi wa Club hii walitengwa. Kadhalika waliohudhuria mkutano mkuu hawakuruhusiwa kuingia na simu za mkononi.
Christopher Karenzi 

Amahoronews.com

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *